YANGA TUNATAKA ROBO FAINALI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi licha ya sare ambayo waliipata dhidi ya Al Ahly lakini bado wanajiona wakiwa na nguvu ya kusonga mbele kwenye kundi lao na kutinga hatua ya robo fainali.

Yanga katika mchezo wa juzi Jumamosi walilazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa.YangaAkizungumza na Championi Jumatatu Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji alisema kuwa “Licha ya kutoka sare katika mchezo huu tunayo kila sababu ya kupambana kwaajili ya kuhakikisha kuwa tunaivuka hatua hii na kutinga hatua inayofuata ya michuano hii.

 

Al Ahly hakuna ambaye hafahamu kuwa hii timu kubwa Afrika lakini ni bingwa mtetezi wa hii michuano mikubwa,baada ya hii sare tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunafanya vizuri katika michezo yetu ijayo ili tusitoke zaidi katika malengo yetu.Yanga“katika kuhakikisha kuwa tunakuwa bora zaidi lazima tukubaliane na ukweli,tutachukuwa maoni na tutarudi tukiwa imara zaidi,kikiubwa ni kufikia malengo yetu na tunawashukuru sana mashabiki wa Yanga kwa sapoti yao kwetu,”alisema Arafat Haji

Acha ujumbe