YANGA KUSHUSHA VYUMA JANUARI

TAARIFA ziwafike mashabiki wa Yanga kuwa kunamashine tatu za maana zitashushwa ndani ya Yanga kupitia dirisha dogo la usajili linatorajiwa kufunguliwa hivi karibuni huku kipaumbele kikubwa kwa Yanga kikiwa ni kwaajili ya michuano ya kimataifa.

Yanga kwa sasa wanashiriki makundi ya ligi ya mabingwa na wanataka kuongeza nguvu kwaajili ya michuano hiyo jambo ambalo linawasukuma kuongeza mashine za kazi.YangaChanzo makini cha kuaminika kutoka Yanga kinasema juu ya mipango ya uongozi wa Yanga na benchi la ufundi la timu hiyo kuhitaji mashine tatu za kazi huku maeneo ambayo yanayotajiwa kuongezewa nguvu ni mshambuliaji wa kati,kiungo wa kati na winga wa pembeni.

“Ni kweli Yanga kupitia bechi la ufundi na viongozi tayari walishajadiliana juu wachezaji ambao wanahitajika ndani ya timu hiyo kupitia dirisha dogo la usajili ambapo kilichobaki kwa sasa ni viongozi kutekeleza.

“Hivyo taarifa zinaeleza kuwa ni nafasi tatu ambazo zimetajwa na benchi la ufundi zinahitaji kuongezewa nguvu ambapo nimshambuliaji wa kati wa maana,kiungo wa kati wa maana wa kusaidiana na Aucho na winga halisia mwenye uwezo mkubwa pia na wakufunga mabao,”kilisema chanzo hiko.YangaKwa mujibu wa taarifa kutoka Yanga rais wa timu hiyo injini Hers Said yeye alisema kuwa “usajili bado haujafunguliwa hivyo kama tumefanya usajili au tutafanya usajili basi mtaona wenyewe kwa kuwa tunasehemu maalumu kwaajili ya taarifa za klabu,lakini cha muhimu ni kuendelea kuipambania timu sisi kama viongozi kwa niaba ya mashabiki na wanachama wa timu hii yetu,”alisema Hersi.

Acha ujumbe