George Mpole Atimkia Lupopo

Mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC msimu uliomalizika George Mpole amesaini mkataba wa kuitumikia klabu ya St Lupopo kutoka nchini Congo.

Mchezaji huyo ambaye alifanya vizuri na klabu ya Geita Gold kutoka mkoani Shinyanga na akafanikiwa kua mfungaji bora wa ligi ya NBC, Lakini mshambuliaji huyo amefanikiwa kusaini mkataba wake na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Congo.george mpoleGeorge Mpole kwa siku za hivi karibuni amekua kwenye mgogoro na klabu yake ya Geita Gold, Huku taarifa zikisema mchezaji huyo aliondoka kwenye kambi kutokana na kutopata uangalifu mzuri wakati anaumwa huku pia akiwa anaidai klabu hiyo.

Mchezaji huyo akiwa na wakala wake wameonekana leo wakirudi Tanzania kutoka nchini Congo ambapo ameshakamilisha dili la kujiunga na klabu ya St Lupopo ya nchini humo, Huku akirudi nyumbani kukamilisha baadhi ya vitu kadhaa.george mpoleMshambuliaji George Mpole ni miongoni mwa washambuliaji waliotabiriwa makubwa sana baada ya kumaliza kinara wa ufungaji kwenye ligi ya NBC msimu uliomalizika, Lakini alianza msimu vibaya na kua na ukame wa mabao kwasasa wadau wanategemea makubwa kutoka kwake baada ya kujiunga na klabu nyingine.

Acha ujumbe