Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United na klabu ya Arsenal Robin Van Persie ameonekana kwenye viunga Carrington ambapo ni uwanja wa mazoezi wa Manchester United.
Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kua mfungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza mara mbili ameonekana kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United akiwa na kocha wa washambuliaji wa timu hiyo Benni Maccarthy.Taarifa zinaeleza Van Persie ambaye alishinda taji moja la ligi kuu ya Uingereza na Manchester United alialikwa na kocha wasasa wa klabu hiyo Eric Ten Hag ambaye ni raia mwenzake wa wa Uholanzi katika viunga hivyo vya Carrington.
Robin Van Persie ambaye anafundisha timu ya vijana ya Feyenoord kwasasa nchini kwao Uholanzi lakini inaelezwa amekuja kujifunza baadhi ya vitu na kuongeza uzoefu ndani ya Manchester United kupitia kocha Eric Ten Hag.