Winga mwenye kasi ya ajabu Tuisila Kisinda Raia wa DR Congo amepigwa Marufuku ya Kuichezea klabu ya Yanga SC kwa kipindi hiki mpaka pale dirisha dogo la usajili litakafunguliwa mwezi Januari, 2022.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kamati ya Sheria, Wanachama na Hadhi za Wachezaji ya TFF, imeamua kwamba Winga huyo Mkongo asuburi mpaka dirisha dogo la usajili ili aweze kujiunga na Yanga SC.
Tuisila alisajiliwa na kutambulishwa na Yanga SC siku ya mwisho wa dirisha kubwa la usajili Agosti 31, 2022 na Klabu hiyo ilimtambulisha usiku wa Giza nene Saa5:59 kabla ya dakika moja tu Dirisha hilo Kufungwa.

Taarifa kutoka klabuni hapo zilisema kuwa, walipeleka jina la mchezaji huyo ili lisajiliwe na Jina la Mshambuliaji wao Lazarous Kambole liondolewe kwenye orodha ya wachezaji wa kigeni wa Yanga SC, kitu ambacho TFF walisema kuwa kisheria haiko sawa kwakuwa Yanga walikwisha chelewa.