Baada ya kuiongoza Mlandege FC kushinda ubingwa wa Mapinduzi Cup 2023, Kocha Mohamed Abdallah ‘Bares’ amesema kuwa tayari ameanza kupokea simu kutoka timu za Tanzania Bara zikiulizia huduma yake. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet.

Katika kuweka mambo sawa Bares amesema yupo tayari kufundisha timu yoyote ikiwa tu watafikia makubaliano!
“Baada ya kumaliza mkataba na JKT Tanzania sikuingia mkataba na timu yoyote, niliamua kurudi nyumbani [Zanzibar] na kwa sasa nafundisha Mlandege FC.”
“Tayari kuna timu zilinifata hata kabla ya Mapinduzi Cup lakini sikuwa tayari. Kwa sasa watu wategemee kuniona Tanzania bara, nawaahidi muda si mrefu wataniona.”
Kocha Bares anayeifundisha Mlandege FC aliwahi kuifundisha JKT Tanzania iliyokuwahi kushiriki Ligi kuu ya Tanzania Bara. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.

Kulingana na mashindano haya ya Kombe la Mapinduzi tayari neema imeanza kushuka kwa baadhi ya wachezaji ambao wamepata fursa ya kusajiliwa na timu kubwa za Tanzania Bara kama vile Mohammed Mussa wa Malindi FC aliyesajiliwa na Simba SC, msimu uliopita Yanga walimsajili Ibrahim Bacca. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa kwenye mechi zote. Bashiri hapa.

