KOCHA mpya wa Yanga Miguel Angel Gamond amesema kuwa kwa sasa jambo ambalo analifikiria ni kuifanya Yanga kutwaa mataji muhimu ili kuendeleza ubora waliouonyesha msimu uliopita.
Yanga msimu uliopita walifanikiwa kutwaa mataji matatu ambayo ni Ngao ya Jamii,Ligi kuu na Kombe la FA.
Kocha huyo raia wa Agentina tayari ametua nchini tayari kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya ambapo wachezaji wanatakiwa kuanza kambi rasmi Julai 10 kesho Jumatatu.
Akizungumza mara baada ya kutua nchini kocha Gamond alisema kuwa “Nimekuja kwaajili ya kuipa Yanga mafanikio,kile ambacho ameniambia Rais wa Yanga ndicho ambacho kimenifanya niweze kushawishika kutua katika hii timu kubwa.
“Jambo kubwa ni Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ndio mlengo mkubwa wa mimi kuwa hapa, naamini kila kitu kitakuwa sawa, ninahamu kubwa kuanza kazi na kuitumikia hii timu.
“Nafahamu kuwa Yanga imepata mafaniko makubwa sna msimu uliomalizika na nafahamu kutakuwana kazi kubwa ya kuhakikisha mashabiki wa Yanga wanafurahi tena kama msimu uliomalizika,tutajitahidi kadri ya uwezo wetu,”alisema kocha huyo.
.

