BAADA ya Simba kukamilisha usajili wa mawinga wawili kiboko Willy Esomba Onana na Aubin Kramo,wameanza tambo kwa kutamba kuwa msimu ujao hawataacha kila kitu kwani watakuwa na wachezaji wa maana.
Simba mpaka sasa imetambulisha usajili wa wachezaji wawili ambo wote ni mawinga wa upande wa kushoto na kulia ambao ni Onana na Kramo jambo ambalo linawafanya kutamba.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmedy Ally alisema kuwa usajili ambao wameufanya kwa msimu huu utawafanya msimu ujao kutimiza malengo yao mapema zaidi na wana uhakika wa kufanikiwa zaidi ya msimu uliopita ambapo majina ya Onana na Aubin Kramo yakitawala mdomoni Semaji.
“Usajili huu tumeufanya kwa umakini mkubwa zaidi na ndio maana unaona kuwa tumeshusha vyuma vya maana tumeanza na mawinga hatari zaidi ambao naamini msimu ujao watatufanya kuwa tishio kweli kweli.
“Simba msimu ujao tunataka kuwa tishio na tunahitaji kubeba kila taji ambalo tutakutana nalo mbele yetu hivyo ndio maana utaona hata usajili tunaoufanya ni waviwango vya juu,bado hatujamaliza na tutashusha vyuma vingine,”alisema kiongozi huyo.

