BAADA ya kufunga bao la kwanza akiwa na uzi wa Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, straika raia wa Ghana Hafiz Konkoni ametoa kauli ya kibabe kwa mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo, akimtaja na Fiston Mayele.
Hafiz Konkoni amesema, lilikuwa na bao ambalo alikuwa analisubiri kwa hamu kubwa kutokana na presha kubwa ambayo alikuwa nayo kutokana na makubwa yaliyofanya na mtangulizi wake kwenye nafasi hiyo ambaye ni Mayele.Hafiz Konkoni aliingia kambani dakika ya 69, ikiwa ni muda mchache aingie akitokea benchi kuchukua nafasi ya Mzambia Kenedy Musonda. Hafiz alisema bila kificho kuwa sasa presha imekwisha na anataka wanayanga wasahau kabisa kuhusu mabao ya Mayele na wayataje mabao yake tu.
“Presha ilikuwa kubwa sana kwangu kutokana na kile ambacho alifanya Mayele kwenye klabu hii kubwa, watu najua wanasubiri kuona nitafanya nini hapa nikiwa na jezi hii.
“Jambo zuri ni kwamba tayari nimeshaanza kazi na nina imani kubwa kuwa, mashabiki watasahau kabisa kuhusu Mayele kutokana na kazi kubwa ambayo nitafanya,” alisema.Yanga walianza msimu wakicheza mechi yao ya kwanza na KMC kwa kishindo, wakifanikiwa kufunga mabao 5-0 kwenye mchezo uliochezwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.