MSHAMBULIAJI wa Simba Saidoo Ntibazokiza, ambaye alitwaa Tuzo ya Mfungaji Bora Msimu uliopita, amefikisha mabao 9 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold Jana.
Simba walikuwa kwenye Uwanja wa Azam Complex wakiwa na harakati zao za kusaka nafasi ya pili na wakafanikiwa kushinda 4-1.Geita walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Geofrey Julius dakika ya 11 na dakika ya 45 bao la kusawazisha kwa Simba lilipatikana kupitia kwa Ntibanzokiza baada ya Shomari Kapombe kuchezewa faulo ndani ya 18.
Saidoo Ntibazonkiza alirejea kambani kwa mara nyingine dakika ya 72 kwa pigo la faulo iliyosababishwa na Willy Onana aliyeingia kipindi cha pili alitokea benchi.
Ladack Chasambi alipachika mabao mawili ilikuwa dakika ya 86 na 90+3 kwenye mchezo huo ambao Geita Gold walishuhudia nyota wao Samuel Onditi akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 63 ikiwa nafasi ya tatu safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 56 sawa na ile ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Yusuph Dabo.
Ikumbukwe kwamba mwamba huyo aliibuka ndani ya Simba akitokea Geita Gold.