Mshambuliaji mpya wa Simba, Augustine Okrah amesema kuwa msimu ujao watakuwa na jambo kubwa la kuhakikisha kuwa Simba inafanya vyema kwa kutwaa kila ubingwa wa mashindano ambayo watashiriki ikiwa ndio mafanikio makubwa zaidi.

Okrah ni ingizo jipya ndani ya Simba akitokea Bechem United ya Ghana,kwa sasa mchezaji huyo yupo katika kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Misri tayari kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao akiwa na timu hiyo.

Okrah alisema kuwa kwa msimu ujao mafaniko makubwa kwao yatakuwa ni kuhakikisha kuwa wanatwaa ubingwa katika kila michuano ambayo watashiriki jambo ambalo anaamini litakuwa furaha kwa mashabiki wote wa timu hiyo.

“Furaha yetu kubwa itakuwa kutwaa mataji yote katika michuano ambayo tutashiriki,sidhani kama kutakuwa na furaha nyingine zaidi ya hiyo na kwa kila mwanasimba atafurahi kusikia tunaweka ahadi hii kwao.

“Najua kuna kazi kubwa haswa kwa wachezaji kama sisi wageni ambao tunahitaji kuonyesha kwanini tulisajiliwa Simba,tutahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa mashabiki ili tufikie malengo yetu,”alisema mchezaji huyo.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa