Kocha wa klabu ya Mancheter United Erik ten Hag amesema bado anahitaji kuboresha kikosu chake kwa kuleta wachezaji wengine wapya kabla ya msimu kuanza.

Mpaka sasa Erik ten Hag amefanikiwa kuwasinisha wachezaji watatu kwenye dirisha hili la kiangazi ambao ni Christian Eriksen, Tyrell Malacia and Lisandro Martinez, lakini bado anaimani atafanikiwa kuwasinisha wachezaji wengine zaidi kabla ya dirisha kufungwa.

Erik Ten Hag, Erik Ten Hag Kurudi Tena Sokoni, Meridianbet

“Tumemsajiri Eriksen kwenye eneo la kiungo, tunafuraha kwa hilo. Na kiukweli nina furaha na kiwango cha eneo letu la kiungo na jinsi wanavyoshambulia kwa sasa.

“Lakini pia najua kuhusu msimu, Kuna michezo mingi ikiwemo kombe la dunia, kwaiyo tunahitaji kuwa na machaguzi mengi unapokuwa na timu nzuri, na sio kuhusu timu tu, pia unahitaji kuwa na kikosi kizuri ili kupata matokeo bora mwisho wa msimu.”

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa