Kocha mpya wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag kwenye mchezo wake wa kwanza katika benchi la timu hiyo ameshuudia  ushindi mkubwa dhidi ya klabu ya Liverpool wa magoli 4-0.

Erik Ten Hag na kikosi cha timu hiyo wapo nchini Thailand kwa ajiri ya kujianda  ya michezo ya pre-season ambapo moja ya michezo hiyo ni wa leo ambao wamekiadhibu kikosi cha Jurgen Klopp goli 4-0  bila hurumu, licha ya nyota wa timu ya United kutokuwepo.

Erik Ten Hag, Erik Ten Hag Aanza na Ushindi wa Kishindo, Meridianbet

Erik Ten Hag  akizungumza baada ya mchezo kuisha alisema, nimeridhika leo. “Timu leo ilikuwa na hamasa kubwa na unajua kuwa ndio kwanza tumeanza. Tulifanya makosa kwenye uchezaji, tumekosa baadhi ya nafasi, lakini tulitengeneza nafasi nyingi.”

Mchezo kati Mashetani wekundu dhidi ya Majoo ya Anfield ulipigwa jijini Bangkok nchini Thailand kwenye dimba la Rajamangala. Magoli ya Manchester United yalifungwa na Jadon Sancho, Fred, Anthony Martial na Facundo Pellistri.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa