Baada tu ya kutambulishwa ndani ya Yanga, Beki Joyce Lomalisa Mutambala amekiri kuwa amekuja ndani ya Yanga kupiga kazi na wala so kuuza sura kwa kuwa anajua nini anatakiwa kufanya kwenye timu hiyo.

Lomalisa unakuwa usajili wanne kwa Yanga kutambulishwa mara baada ya kutangulia kutambulishwa kwa wachezaji Lazarous Kambole, Bernard Morrison na Gael Bigirimana.

Lomalisa anayemudu kucheza katika nafasi ya beki wa kushoto ambapo amesajiliwa kutoka katika klabu ya Sagrada Esparanca ya nchini Angola na ni mchezaji mwenye rekodi nzuri kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya DR Congo.

“Nimekuja Tanzania kufanya kazi na wala sio kuuza sura, najua kila kitu kuhusu Yanga na bahati nzuri kuna ndugu zangu wengi hapa Yanga kutoka DR Congo naamini watanipa ushirikiano mzuri.”

“Mimi kujiunga na Yanga inatokana na mahitaji ya timu, kiu yao ya kuhitaji kufanya vyema katika michuano ya kimataifa imechangia kwa ukubwa mimi kuwepo hapa,” alisema.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa