PENGINE muda wowote beki wa kushoto wa Simba Gadiel Michale atatambulishwa kuwa mchezaji wa Singida Big Stars kwa mkopo wa mwaka mmoja kwa mujibu wa taarifa za mmoja wa viongozi wa timu hiyo.

Mtoa taarifa hiyo alisema kuwa makubaliano kati ya mchezaji na klabu tayari wameshafikia pazuri kinachosubiriwa ni uongozi wa Simba wakubali kumuacha mchezaji huyo kwa kuwa ofa tayari imeshakwenda mezani kwao.

Simba, Beki Simba, Singida Big Stars Mambo Safi, Meridianbet

Kiongozi huyo alisema, wanaweza kumtambulisha Gadiel kama mambo yatakwenda sawa kwa kuwa makubaliano baina ya timu na mchezaji yamefikia pazuri na wanachosubiriwa ni viongozi wa Simba kumuachia.

“Muda wowote tunaweza kumtangaza Gadiel kwa sababu viongozi wameshafanya naye mazungumzo na wameshakubaliana. Simba wakiruhusu basi atacheza kwetu kwa mkopo,” alisema mtu huyo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Big Stars, Hussein Masanza ili kujua ukweli wa taarifa hizo alisema: “Bado tunaendelea na zoezi la usajili. Kama naye yupo kwenye mkeka tutamtangaza tu muda ukifika.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa