YANGA MPANGO WAO WA PARADE LA UBINGWA UPO HIVI

MABINGWA mara 30 wa Ligi Kuu Bara Yanga wamebainisha kuwa kutakuwa Parade la Ubingwa la maana Mei 26 2024 ambalo litaanzia Uwanja wa Mkapa asubuhi mpaka Jangwani.

Ipo wazi kwamba Yanga metwaa ubingwa baada ya kucheza mechi 27 ikifikisha pointi 71 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ndani ya ligi msimu wa 2023/24. Hivyo vita yam mbio za ubingwa zimefungwa kilichobaki ni kuwania nafasi ya pili pamoja na vita ya kushuka daraja.YangaAli Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa kwenye mpango kazi wao huo watapita kwenye vituo mbalimbali ambavyo vinajulikana ikiwa ni pamoja na Msimbazi ambapo hapo yalipo makao ya watani zao wa jadi Simba amebainisha kuwa hawatapita tu bali watakaa.

“Mnamo tarehe 26 Mei 2024 tutakuwa na Parade la Ubingwa. Tutaanzia Uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia asubuhi kuja Jangwani. Najua miongoni mwa vituo vyetu mnavijua. Safari hii hatupiti tu, tutakaa hapo kwa muda.

“Kabla ya Parade la Ubingwa siku ya Jumapili (25 Mei) tunatarajia kuwa na Supu Day ya kusherehekea Ubingwa hapo hapo Lupaso. Tumeshapata ahadi ya ng’ombe sio chini ya 8 hadi hivi sasa.

“Mchezo wa tarehe 25 Mei 2024 dhidi ya Tabora United, Yanga tutakabidhiwa Ubingwa wetu na wadhamini wetu NBC, mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa Mkapa.

“Siku nzima Wananchi tunapaswa kutamba na kuvimba, mageti yatafunguliwa saa tano asubuhi. Kutakuwepo na burudani kutoka kwa wasanii wakubwa kuanzia saa tano. Hivyo itakuwa ni siku ya burudani kwa kila mmoja.Yanga“Kwenye mechi ya kukabidhiwa Ubingwa dhidi ya Tabora tutakuwa na jambo kubwa na la kihistoria kwenye mechi za kukabidhiwa Ubingwa katika nchi hii. Mwananchi ukikosa hii surprise ya kipekee basi ujilaumu wewe mwenyewe. Popote ulipo anza safari uje kwenye Jumamosi ya Kibingwa.

“Siku ya kukabidhiwa Ubingwa tutakuwa na MaDJ watakaokuwepo. Kuanzia leo tutaanza kutaja orodha ya MaDJ watakaotupatia burudani ya Ubingwa akiwemo DJ Ally B. Tutataja na wasanii wakubwa ambao tutawashusha kwa Mkapa.”

Acha ujumbe