SIMBA SC siku ya Jumapili watashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki na Malindi SC kwenye uwaja wa Aman Zanzibar na kisha Septemba 28 watacheza na Kipanga FC ikiwa ni michezo ya kirafiki kwa kadi ya mualiko ya Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF).

Awali Michezo hiyo ilipangwa kuchezwa tarehe 25 Septemba ambapo angeanza na Kipanga FC na Tarehe 27 wangecheza na Malindi SC.

 

Mabadiliko ya Mechi za Simba.

Nafasi hiyo ya kupata mechi hizo, imemfungua mdomo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally na kusema kuwa mechi hizo mbili kwao ni faida kubwa kwani kocha Juma Mgunda atapata nafasi kukaa zaidi na timu yake kabla ya mechi za mashindano kurejea.

Ahmed alisema: “Mechi hizi za mualiko wa ZFF tumezipokea kwa furaha sana kwa sababu moja kwa moja zinakwenda kumpa nafasi mwalimu wetu Mgunda kukaa zaidi na wachezaji na kuwaandaa kabla ya mechi muhimu za hatua yakwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Mabadiliko ya Mechi za Simba.
Ahmed Ally-Afisa Habari na Mawasiliano wa Simba SC

“Kipanga wao ni washiriki wa Kombe la Shirikisho Afrika na Malindi pia ni moja ya timu bora kule Zanzibar, kwahiyo watatupa ladha halisi ya kimashindano na tunakwenda kucheza kweli mechi hizo.”

Simba SC wataondoka kesho Jumamosi kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mechi hizo na wakiondoka na wachezaji wote muhimu isipokuwa wale walio na majukumu ya timu za taifa.

 

Mabadiliko ya Mechi za Simba.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa