Sergio Busquets kiungo na nahodha wa klabu ya Fc Barcelona na timu taifa ya Hispania ameweka wazi kufikia mwisho wa msimu huu ndo itakua mwisho wa kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake jijini Barcelona.

Kiungo huyo zao kutoka kwenye timu ya vijana ya Barcelona maarufu kama La Masia ameitumikia timu hiyo takribani miaka 15 huku akibaki kama gwiji na mchezaji aliepata mafanikio makubwa klabuni hapo pamoja na timu ya taifa ya Hispania.

busquetsKiungo huyo amekua mhimili kwenye kikosi cha dhahabu cha Barcelona na timu ya taifa ya Hispania vilivyopata mafanikio makubwa huku yeye akiwa na mchango mkubwa kwenye vikosi hivyo.

Busquets amekua kwenye kikosi cha Barcelona kilichobeba mataji matatu kwa msimu mmoja mara mbili maarufu kama (Trebble) huku akiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kilichobeba kombe la dunia 2010 na kombe la ulaya 2012 huku akiwa nguzo katika eneo la kiungo wa chini.

Kiungo huyo mwenye miaka 34 amepata mafanikio binafsi pia kama kuingia kwenye kikosi bora dunia mara kadhaa, kikosi bora cha mwaka La liga,amefanikiwa kuingia kwenye timu bora ya michuano ligi ya mabingwa ulaya msimu wa 2014/15, mchezaji bora chipukizi wa La liga mwaka 2009 haya ni miongoni mwa mafanikio binafsi ya Sergio Busquets.

busquetsSergi anakua mchezaji wa mwisho kuondoka klabuni hapo katika utatu wa viungo wa klabu hiyo uliitikisa dunia katika miaka ya 2009 mpaka 2015 akiwa na magwiji kama Xavi kwasasa kocha wa Barca pamoja na Andres Iniesta anayecheza nchini China.

Sergi atakumbukwa kama kiungo wa ulinzi mwenye maarifa makubwa zaidi kuwahi kucheza soka kutokana na namna yake ya uchezaji ya kuweza kukaba kwa maarifa na kuichezesha timu kuanzia chini na uwezo wake wa kuweza kumiliki dimba.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa