MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania anayecheza kwenye klabu ya Ligi Kuu Sweeden BK Hacken Aisha Masaka anasema anashukuru Mungu kuwa kila kitu kinakwenda sawa kwenye maisha yake ya Ulaya.
Hivi karibuni Masaka alikuwa nje ya uwanja akisumbuliwa na majeraha ya bega ambayo kwa mujibu wake mwenyewe kuwa anaendelea vizuri kwenye kila kitu chake akiwa nchini Sweeden.
“Naendelea vizuri sana kwenye kila kitu, mchezaji kupata majeraha ni jambo la kawaida na nilipata kweli na mambo yapo sawa kwa sasa hakuna shida yoyote,” alisema.
Masaka anacheza msimu wake wa pili BK Hacken, ingawa bado hajapata wakati mzuri wa kucheza kwenye kikosi cha kwanza, licha ya kuwa kuna baadhi ya mechi alikuwa akianza na zingine akianzia benchi.

