MAXI ATOA KAULI YA KIBABE

LICHA ya kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara mwezi Agosti, bado kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani, Maxi Nzengeli amesema ana mengi mazuri aliyopanga kuifanyia timu hiyo msimu huu.

Staa huyo ambaye ameshinda tuzo hiyo akiwashinda Jean Baleke wa Simba na kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki, kwa mwezi Agosti akicheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara, amefunga mabao mawili na asisti moja.MAXIMaxi alisema tuzo hiyo imemuongezea hamasa na hali ya kujituma akiwa uwanjani kuipambania timu yake.

 

Maxi alisema ana deni kubwa la kulilipa ndani ya Yanga, kama sehemu ya kuwashukuru mashabiki wa timu hiyo, kutokana na mapokezi, sapoti kubwa wanayompa akiwa uwanjani.

“Niwashukuru mashabiki kwa sapoti kubwa ambayo wamekuwa wakinipa uwanjani, hiyo ndio imenipa hamasa ya mimi kuipambania timu yangu na kufanikiwa kushinda kuwa mchezaji bora wa Agosti.

“Ninataka kuona nikiendelea na mwendelezo mzuri katika michezo yote iliyokuwepo mbele yetu, hiyo itaiwezesha timu kupata matokeo mazuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu.MAXI“Haitakuwa rahisi kwangu mimi kufanya vizuri, bila ya sapoti ya mashabiki na wachezaji wenzangu, nawaomba mashabiki waendelee na moyo kwangu, kwani bila yao sio chochote kwangu,” alisema Maxi.

Acha ujumbe