Stori ya Wayne Rooney kutoka Everton Kwenda Manchester United ilikuwa na utamu wake. Ilikuwa na kila uzuri, pale Old traford palimtii Wayne.
Wajukwaa yakaimba jina lake, lakini ile damu yake ya Mercessayd inaweka dosari kubwa sana. Ule u-everton wake unamnyima heshima anayopaswa kuipata.

Lakini njoo nikuambie kuhusu stori ya Anko aliyezaliwa Jiji la miamba, alafu akazaliwa tena mitaa ya twiga na Jangwani.
Kisha akaifanya mitaa hii kuwa nyumbani kwake rasmi. Zile ondoka rudi, ondoka rudi za anko pale yanga zinathibitisha maneno hayo.
Natamani Anko anifundishe ujasiri na Mapenzi yaliyopitiliza kwa kubusu shavu la mke wake wa zamani huku akiwa amemkumbatia mke wake mpya!
Nakumbuka alichokifanya ile siku anaibusu jezi ya Yanga akiwa mchezaji wa Azam? endless love.
Mrisho Ngasa mmoja tuu ndie niliwahi kumuona Mbele ya Camera na Maiki za waandishi, akiahidi kuwafunga watani wao wa jadi Simba, na kwa kujiamini akaahidi asipofunga nyumba yake ichomwe moto Mitaa ya DSM.

Mrisho Ngasa aliamua kuzaliwa upya Mitaa ya Jangwani na hapa pakawa nyumbani kwake, majukwaa yalimuimba na kumshangilia.
Utazungumza nini kuhusu Anko na usizungumze kuhusu Yanga, hii ilikuwa ndoa ya watu walioshibana haswaa, wakigombana kashike jembe ukalime.
Ile sajili yake kwenda Simba ilikuwa kujenga historia ya kupita kotekote tuu, nadhani uliona nini kilitokea baada ya msimu mmoja mbele.
Moyo wa mrisho una vyumba vyake vitano, usishangae, kingine kinachoongezeka ni kile cha kijani na njano.

Makombe saba na jezi ya kijani, ufungaji bora mara kadhaa. Kubwa ni ile tuzo ya ufungaji bora wa CAF CL 2014 mabao 6, yuko sawa kitakwimu na Mbwana Sammata kuchukua tuzo hii.
Hayo yote ni akiwa na uzi wa kijani na Njano. Kwenda Seattlesounders walimuita akacheze na Man united Ya Fergie akitokea Jangwani, Usisahau Ile stori ya kwenda Westham.
Imeandikwa na Stive Njema
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!