Klabu ya Arsenal imegoma kumuachia mchezaji wake Hector Bellerin kujiunga na klabu ya Hispania Real Betis kwenye uhamisho huru kufuatia kuwa na msimu wenye mafanikioa kwenye klabu hiyo aliyokuwa akiicheza kwa mkopo.
Hector Bellerin ambaye alikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye klabu ya Arsenal na ili aweze kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara alipelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Real Betis majira ya kiangazi yaliopita.

Hector Bellerin amekuwa na msimu bora na klabu ya Real Betis, amefanikiwa kucheza michezo 32 kwenye mashindano yote na allifanikiwa kutoa pasi ya goli kwenye mchezo wa fainali ya Copa Del Rey na pia alicheza kwa dakika 120 kwenye mchezo wa ushindi dhidi ya Valencia.
Real Betis wanataka kufanya usajiri wa jumla na kumchukua moja kwa moja Bellerin lakini mpaka sasa bado hawajafanya mazungumzo yoyote wala kuulizia thamani yake kwenye klabu ya Arsenal.

Kulinga na Estadio Deportivo kupitia Daily Mail, Imeripoti kuwa Arsenal hawana nia ya kuvunja mktaba na kumwachia aende huru kwenye klabu yoyote, lakini wako tayari kupokea kiasi cha ada au ubadilshanyaji wa mchezaji kwa mchezaji
Ukiondoa klabu ya Betis, kuna klabu kadhaa nazo zinahitaji huduma yake ambazo ni , Fiorentina, Juventus na Inter Milan na vili vile klabu ya Barcelona ambayo inatizama maendeleo ya mchezaji huyo.
Hector Bellerin anataka kubaki kwenye klabu ya Betis, na pia yuko tayari kupunguuza mshahara wake wa £100,000 kwa wiki ili aweze kurahisisha uhamisho huo, mwezi uliopota aliiambia Betis TV.
Nimeweshaweka wazi nafasi yangu kwa klabu zote mbili, na sasa tuna miezi miwili ya kufanikisha uhamisho kwa pande zote tatu. Mara zote nimesema , nimefanya juhudi kuja hapa na nina ya kutaka kufanya kila liwezekanalo nibaki hapa, sababu ni nyumbani na nina furaha.
Ni kweli nilikuwa na kipindi bora London, Arsenal walinipa nafasi nyingi ya kuwa professional. kama nitaondoka, itakuwa ngumu , lakini natumai kila kitu kitakwenda vizuri kama tunavyotaka.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!


