Kocha wa klabu ya AS Roma na mshindi wa UEFA Conference League Jose Mourinho ameweka wazi kuwa klabu hiyo imemfanya kutojofikilia yeye zaidi tofauti na alivyokuwa hapo awali.

Mourinho ambaye alijipa jina la “The Special One” akiwa kwenye klabu ya Chelsea hakuwa na misimu mizuri ya hivi karibuni kwenye klabu za Manchester United na Tottenham Hotspur kabla ya kujiunga na klabu ya Roma na kufanikiwa kuipa uningwa wa kwanza wa ulaya.

Jose Mourinho

“Imenifanya nijisikie tofauti juenda sijawai kujisikia hivi kabla, ni kama ilikuwa ubingwa wa ulaya kwetu,” Mourinho aliwaambia wanafunzi wa University of Lisbon.

“Sijisikii tena kuwa mbinafsi tena, nimekuwa mtu wa kuisha maisha ya wengine zaidi kuliko yangu mwenyewe.”

Pia Jose Mourinho alikubali kuwa kuna baadhi ya wachezaji ambao walifanikisha safari ya hiyo ya ubingwa hawatakuwepo kwenye kikosi hicho kwa msimu ujao, mmoja wapo ni Sergio Oliveira ambaye alikuwa anaichezea klabu hiyo kwa mkopo akitokea Porto, huku kukiwa na kipengere cha kumnunu chenye thamani ya  €13m, lakini Roma haina nia ya kulipa pesa hiyo.

“Ikiwa Porto watataka tena kumtoa kwa mkopo tena kwetu, mimi binafsi nitamrudisha Roma. Ikiwa kuhusu swala la kumnunua, basi sidhani kama credit card yangu itaweza kutumika,” Mourinho alijibu alipoulizwa kuhusu Olivera.

“Alikuwa mchezaji wa muhimu msimu huu, tumekuwa na kanuni nyingi ambazo unahitaji kwenye soka na zimenisaidia kufikia ujumbe kwa wengine. Ameonyesha mfano tuliokuwa tunahitaji.

“Ningependa abaki, lakini itatubidi tusubiri tuone.”

Jose Mourinho kwa sasa ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza, kufanikiwa kuchukua makombe yote ya Ulaya ngazi ya klabu kuanzia UEFA Champions League, UEFA Europa  League na UEFA Europa Conference League.

Jose Mourinho alimwaga machozi ikiwa ni nadra kwa mreno huyo kufanya hivyo, alpofanikiwa kuipa ROMA ubingwa wa kwanza wa Ulaya wa UEFA Europa Conference League.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa