Kocha wa klabu ya Yanga Nasserdine Nabi amelalamikia ratiba ya ligi kuu Tanzania Bara kuelekea mchezo wao wa kombe la shirikisho dhidi Club Africain kutoka nchini Tunisia.
Kocha huyo wa klabu ya Yanga amelalamikia kua ratiba ya Ligi kuu nchini imekua ngumu na kusababisha kukosa muda wa kujiandaa vizuri dhidi ya Wapinzani wao hao kutoka nchini Tunisia ambapo ni nyumbani kwa kocha huyo kiasili.
Klabu ya Yanga imecheza michezo takribani minne ndani ya siku chache kitu ambacho mwalimu Nabi amekilalamikia,Pia kusababisha majeraha kwa baadhi ya wachezaji wawili kwenye kikosi chake kutokana na kucheza michezo mingi ndani ya siku chache.
Nabi amekua kocha wa pili amekua wa klabu hiyo kulalamikia ratiba ngumu hapo mwanzo kocha msaidizi wa klabu hiyo Cedric Kaze pia alilalamikia ratiba kuwabana klabu hiyo kuelekea mchezo wao wa kimataifa. Mwalimu Kaze yeye aliamini shirikisho lilipaswa kuwasaidia Klabu hiyo na kuwapa muda wa kupumzika kwakua wanawakilisha taifa.
Kocha huyo amezungumza na waandishi wa habari leo hii kuelekea mchezo wa dhidi ya Club Africain ambao utapigwa kesho katika dimba la Benjamin Mkapa, Amesema hawezi kutumia sababu ya ratiba lakini ukweli hawapata mda wa kujiandaa zaidi wameweza tu kumsoma mpinzani wao.

