Klabu ya Ac Milan na mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Italia wamefanikiwa kumuongezea mkataba mpya kocha wao wa sasa Stefano Pioli mpaka 2024.
Kocha huyo ambaye amedumu klabuni hapo kwa takribani misimu minne na kufanikiwa kuwapa taji la ligi kuu nchini Italia baada ya miaka 11. Hiyo ni miongoni mwa mambo ambayo yameweza kuwavutia mabosi wa Milan kumuongozea mkataba kocha huyo.
Klabu ya Ac Milan ambao walipoteza nguvu katika soka la Italia pamoja na ulaya kwa ujumla lakini chini ya mwalimu Stefano Pioli wamefanikiwa kuanza kuurudisha utawala wao.
Kocha Pioli kocha wa zamani wa vilabu vya Inter Milan, Fiorentina, na Lazio amekua ni miongoni mwa makocha wenye ubora ndani ya ligi kuu ya Italia kutokana na namna ameweza kuisuka klabu ya Ac Milan ambayo ilikua kwenye hali mbaya zaidi miaka kadhaa nyuma.
Kocha huyo ambae alikua anamaliza mkataba wake hivi karibuni lakini klabu ya Ac Milan imeona kocha huyo anafaa kuendelea kukinoa kikosi hicho kutokana na ubora inaouonesha na kumuongezea mkataba mpya mpaka juni 2025.

