Kikosi cha Polisi Tanzania tayari kimerejea mazoezini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya KMC.

Polisi Tanzania wanatarajia kucheza mchezo huo Desemba 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga kwa mabao 3-0.

Polisi wasahau kipigo cha Yanga

Akizungumzia mipango yao, Kocha Msaidizi, John Tamba amesema “Tayari kikosi chetu kimeendelea na maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya KMC.

“Tayari tumesahau yale yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Yanga hivyo kwa sasa tunajiandaa na mechi ya KMC kwa ajili ya kutafuta pointi tatu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa