Mshambuliaji wa klabu ya Azam ambaye ameandika barua ya kutaka kuondoka klabuni hapo Prince Dude amefunguka makubwa ambayo yamewashtua wengi, Huku kubwa likiwa kuwashtumu viongozi wa timu hiyo kuwahujumu.
Mshambuliaji huyo amefunguka mambo mengi lakini kubwa ni kuwashutumu viongozi wa klabu hiyo kuwahujumu, Kwani amesema viongozi wa timu hiyo wamekua wakishabikia timu zingine za nje ya timu hiyo jambo ambalo muda mwingine limekua likiwafelisha.“Sikutaka kusema lakini imefika muda inanibidi tu niseme, ndani ya timu kuna watu tena viongozi wa juu walikua wakituhujumu. Haiwezekani viongozi wa ngazi za juu Wanakutwa wanashabikia timu zingine tena bila hata kujificha, timu zingine zikishinda wanafurahia. Hivi unajua ni ngumu kiasi gani wewe upo kwenye timu ambayo mnapambana mshinde kitu lakini viongozi wanaowaongoza wanasapoti timu mnayoshindana nayo, ndio maana nataka mabadiliko, niende sehemu ambayo watu wote mnawaza na kufikiria kitu kimoja” Prince Dube akishutumu uwepo wa Baadhi ya viongozi wa Azam kushabikia na kusapoti timu zingine nje ya Azam..
“Nilivyojiunga na Azam Fc nilikua na malengo na matumaini makubwa maana nilidhani hii ni timu kubwa ambayo ingeweza kushindana na cv yangu kuongezeka. Pamoja na mambo kwenda kinyume na vile nilivyotarajia lakini niliendelea kujipa moyo kua mambo yatakaa sawa lakini kadri siku zinavyozidi kwenda ndio naona hali ya timu inazidi kua mbaya zaidi. “Unaweza kuona msimu ukianza hua tunaanza vizuri sana lakini unaona mambo yanabadilika ukichunguza kwa makini huoni shida yetu( wachezaji) Ila mambo yanakua mabaya tu kibaya hakuna anayejali Dhamira yangu nikucheza kwenye ushindani na kushinda kwaajili ya timu yangu na kuona timu inasonga mbele kitu ambacho kwa hapa hakipo sijui kwa siku zijazo japo sidhani kama kinaweza kutokea hivi karibuni”Alisema Prince Dube