Klabu ya soka ya Simba imebanwa mbavu jijini Mbeya baada ya kulazimishwa sare ya goli moja kwa moja na klabu ya Mbeya City katika mchezo uliopigwa katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.

Klabu ya Simba ndio ilifanikiwa kupata goli katika kipindi cha kwanza baada ya kiungo wake Muzamiru Yassin kufunga bao la kuongoza na mpaka mpira unaenda mapumziko klabu ya Simba ilikua mbele kwa moja kwa bila.simbaMchezo huo ambao ulkua wa kasi kwa pande zote mbili ambapo klabu ya Mbeya City ilionesha upinzani wa hali ya juu mbele ya Wekundu wa msimbazi mpaka pale Tariq Seif alipoisawazishia klabu ya Mbeya City dakika ya 79 na mchezo kumalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Klabu ya Simba imekua kwasasa imesali nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kufikisha alama 28 ikiwa imecheza michezo 13 huku Yanga wakiwa na alama 29 wakiwa na michezo 11 kwenye nafasi ya kwanza huku klabu ya Azam wao wakiwa nafasi ya pili wakiwa na alama 29 kwa michezo 13.simbaWekundu wa msimbazi wanaonekana kuchechemea kwa msimu wa pili sasa kwenye ligi kuu baada ya kubeba ubingwa huo mara nne mfululizo huku kelele za mashabiki wa klabu hiyo wakianza kutoa lawama kwa viongozi wa juu ya mwenendo wa timu yao.

machaguo spesho

Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa