Kiungo wa klabu Manchester United na timu ya taifa ya Ureno Bruno Fernandes ameeleza kucheza na aliekua mchezaji mwenzake wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo ilikua ni ndoto yake.
Kiungo huyo ameyaongea hayo baada ya mchezaji huyo kumalizana na mashetani wekundu siku ya jana ikiwa bado haijafahamika mchezaji huyo ataibukia klabu gani baada ya michuano ya kombe la dunia.Kuondoka kwa Ronaldo kulionekana hakuepukiki baada ya kufanya mahojiano na mtangazaji mkubwa nchini Uingereza Piers Morgan na kueleza mambo mengi ikiwemo mahusiano yake na kocha wa sasa wa klabu hiyo Ten haag huku pia akiweka wazi Uongozi wa klabu hiyom unavyoikwamisha klabu hiyo.
Bruno Fernandes alipoulizwa kuhusu kuondoka kwa nyota huyo klabuni hapo alisema atathamini kipindfi chote walichokaa pamoja ndani ya klabu hiyo huku akiweka wazi ilikua ni ndoto yake kucheza timu moja na gwiji huyo wa soka duniani.
Siku kadhaa nyuma ilionekana kua Ronaldo na Bruno walikua na tofaut jambo ambalo wote kwa vipindi tofauti walikanusha walipohojowa na kusema wako sawa na hawana tofauti zozote baina yao.Bruno Fernandes na Ronaldo wote wapo kwenye timu ya taifa ya Ureno ambayo inajiandaa kucheza mchezo wao wa kwanza wa michuano ya kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Ghana hapo kesho huku mchezaji huyo akisisitiza wao kama timu malengo yao kwasasa ni timu ya taifa.
Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.
BONYEZA HAPA