Kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba SC ambao utafanyika mwakani Tarehe 29 Januari 2023, Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Boniface Lyamwike amesema kuwa watatumia kanuni za klabu na sio zile za TFF zilizokuwa zinatumika miaka ya nyuma.
Lyamwike amesema hayo alipokuwa anazungumzia maandalizi ya uchaguzi huo leo Jijini Dar Es Salaam.
“Mwaka huu kanuni ambazo zitatumika kwenye uchaguzi wa Simba ni kanuni za Simba Sports Club. Huko nyumba tulikuwa tunatumia kanuni za TFF, katiba ya Simba ilikuwa inaruhusu.”- Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Simba, Boniface Lyamwike.
Kanuni hizo alizozitaja zilipitishwa kwenye katiba mpya ya Klabu hiyo, ambayo ilipitishwa ili kurahisisha zoezi la uwekezaji ambapo kanuni za uchaguzi huo zinawataka wagombea kuwa ni wanachama halali wa Simba SC.
“Kanuni ya sita (kanuni za uchaguzi Simba), kigezo cha kwanza mgombea lazima awe mwadilifu na awe na kiwango cha juu cha uaminifu. La pili lazima awe mwanachama hai wa klabu.”
“Mtu yeyote ambaye anagombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ni lazima awe na angalau shahada ya chuo kikuu, na lazima awe na uwezo na haiba ya kuwakilisha klabu ndani na nje ya nchi.”
Awali Uchaguzi huo ulipaswa kufanyika mwaka huu, lakini Uongozi wa Simba ulikubaliana kuupeleka mpaka Januari 29, mwaka 2023. Utahusisha upatikanaji wa Uongozi mpya.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.



