KOCHA Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nassredine Nabi amewaonya mastaa wake kucheza kwa tahadhari na kutokuumizana kulingana na ratiba ngumu ya michezo mingi ya kimataifa na ligi kuu huku pia wakitarajiwa kucheza michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Yanga kwa sasa ndio vinara wa ligi kuu lakini pia wanashiriki Kombe la Shirikisho Afrika wakipangwa Kundi D sambamba na klabu za TP Mazembe ya DR Congo, US Monastir ya Tunisia na Real Bamako ya Mali.

Wachezaji Yanga watahadharishwa

Kocha Nabi alisema, jambo kubwa ambalo anawasihi wachezaji wake ni kucheza kwa makini na kulindana hata wakiwa mazoezini ili wasije wakaumiza na mwisho wa siku wakapatwa na majeraha yatakayowafanya wakose baadhi ya mechi muhimu.

“Tuna michezo mingi sana inakuja mbele yetu, tuna michuano mingi kuanzia ligi kuu, Shirikisho Afrika na Shirikisho la Azam kwa maana ya FA lakini pia tuna michuano mingine itafuata ya Mapinduzi Cup utaona ni kwa namna gani kutakuwa na mechi nyingi sana zilizopo mbele yetu.

Wachezaji Yanga watahadharishwa

“Ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuhakikisha kuwa wachezaji wanacheza kwa tahadhari kubwa sana kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi zetu ili wasije wakapatwa na majeraha.

“Kulingana na wingi wa mechi uliopo mbele yetu lakini malengo ni yale yale katika kila michuano lazima tuwe bora zaidi ya wengine na tuweze kupata matokeo mazuri,” alisema kocha huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa