Rais wa shirikisho la soka duniani Gianni Infantino ametangaza rasmi michuano ya kombe la dunia ngazi ya klabu itakua na timu 32 kuanzia mwaka 2025.

Rais huyo ameeleza hayo wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari nchini Qatar ambako michuano ya kombe la dunia inafanyika mwaka huu. Kwa kawaida kombe la dunia la Vilabu limkua likishirikisha timu sita ambazo zinakua mabingwa katika kila bara.infantinoRais Infantino amesema kuanzia mwaka 2025 kipindi cha majira ya joto na kusema kutakua na timu 32 shiriki kwenye michuano hiyo kwenye kila miaka minne, Na kuongeza kua watakua wanaalika timu bora duniani kushiriki michuano hiyo.

Wakati akifanya mahojiano hayo Rais huyo ameonesha kua michuano hiyo itakua inachezwa kama ngazi ya timu ya taifa yaani kila baada ya miaka minne michuano hiyo itakua inapigwa na kushiriisha timu 32 kutoka duniani kote.infantinoInfantino pia ameeleza kua suala la timu kuongozeka kwenye kombe la dunia ngazi ya taifa kama ambavyo ilielezwa hapo awali, Rais huyo ameweka wazi kua kombe la dunia la ngazi ya taifa kuanzia michuano ya kombe la dunia lijalo timu zitakua 48.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa