Yanga Kesho ni Kufa na Kupona

YANGA SC iliyoweka kambi yao kwenye mji wa Sousse nchini Tunisia, imewafuata Club Africain mapema sana kwenye mji wao wa Tunis kwaajili ya mchezo wa marudiano mkondo wa pili, kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.

Mji huo wa Tunis ndio sehemu ambapo mchezo huo wa kukata na shoka utapigwa, kwenye dimba la Olympique Hamad Agrebi majira ya saa 2:00 usiku kwa majira ya Tanzania.

 

Yanga Kesho ni Kufa na Kupona

Yanga SC ukiangalia kikosi chake na uwezo wa mchezaji mmjoa mmoja, wana uwezo wa kushinda mechi hiyo kwani mechi iko wazi kwa kila upande, ukizingatia Yanga inahitaji hata sare ya magoli ya idadi yeyote isipokuwa sare ya kutokufungana 0-0, itawalazimu kwenda kwenye mikwaju ya penati.

Mtazame Stephen Aziz Ki uwezo wake wa kutengeneza nafasi, kupiga mipira ya kutenga na uwezo wake wa kupiga nje ya boksi, Rudi kwa Feisal Salum kiungo mnyumbulifu mwenye uwezo mkubwa wa kupiga akiwa mbali na shabaha ya kulenga goli.

 

Yanga Kesho ni Kufa na Kupona

Tazama uwezo wa Morrison akiwa kwenye kiwango kizuri anaweza akaipa timu matokeo, rudi kwa Mayele ni mshambuliaji anayejua jinsi ya kutumia nafasi kufunga pindi anapoipata. Safu ya kiungo ya Yanga imekamilika Khaleed Aucho, Salum Abubakar, Yannick Bangala bado Yanga wako vizuri sana.

 

Yanga Kesho ni Kufa na Kupona

Tutegemee kuiona mechi ngumu itakayoamuliwa na uwezo wa mchezaji pamoja na mbinu za Mwalimu Nabi, Ila Club Africain kwa upande wao sio wabaya wana uwezo wa kushambulia kwa nguvu na kukaba kwa akili nyingi, na huwa wanabadilika sana pindi wanapokuwa nyumbani.

Acha ujumbe