Beki wa klabu ya Geita Gold ya mkoani Geita Kelvin Yondani anatajwa kufikia hatua za mwisho kumalizana na wakata miwa wa mkoani Kagera klabu ya Kageta Sugar.

Yondani ambaye ameitumikia klabu ya Geita kwa Takribani kipindi cha mwaka mnoja baada ya kujiunga na timu hiyo kwenye dirisha dogo lililopita akitokea klabu ya Polisi Tanzania ya mkoani Kilimanjaro. Hivo akifanikiwa kuandoka klabuni hapo majira haya anakua ameitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.

Klabu ya Kagera Sugar inamuhitaji Yondani kwajili ya kuimarisha safu yao ya ulinzi ambayo imeonekana kua kwenye hali mbaya zaidi msimu huu. Klabu ya Kagera Sugar imekua moja ya vilabu vilivyoruhusu mabao mengi zaidi msimu huu wakifanikiwa kuruhusu mabao 22 ndani ya michezo 19 waliyocheza mpaka sasa.YondaniKelvin Yondani kama dili lake la kujiunga na klabu ya Kagera Sugar likikamilika basi anaongeza idadi ya rundo la wachezaji walioachana na klabu ya Geita gold kipindi hichi cha dririsha dogo, Kwani mpaka sasa klabu hiyo imeondokewa na nyota wake wasiopungua sita.

Beki Yondani ambaye amewahi kukipiga pia klabu ya soka ya Yanga kwa mafanikio makubwa kama ataondoka kwenye klabu ya Geita basi litakua pigo kubwa, Kwani beki huyo amekua mhimili mkubwa kwenye safu ya ulinzi ya klabu hiyo tangu ajiunge klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa