Staa Kylian Mbappe amepata sapoti kutoka kwa kocha wake wa klabu ya PSG baada ya kumtolea uvivu Rais wa shirikisho la soka Ufaransa juu kumkosea heshima Zidane.

Siku chache zilizopita rais wa shirikisho la soka Ufaransa Noel La Graet aliibua mijadala mbalimbali kutoka kwa wadau wa mpira wa miguu ikiwemo Mbappe baada ya kuonekana kukosea heshima gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Zinedine Zidane.MbappeRais La Graet alizungumza kua hajali kuhusu Zidane kujiunga na timu ya taifa ya Brazil na na kusema kua pia gwiji huyo hakumpigia simu kumuulizia kibarua cha kua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa, Lakini Rais huyo amesema hakupata simu ya Zidane na hatakama angepiga asingepokea vilevile.

Kauli ya Rais huyo iliiibua mijadala sana huku Mbappe kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter aliandika “Zidane ni Ufaransa, Hatuwezi Kumkosea Heshima kwa namna hiyo” Haya yalikua maneno ya staa huyo kuonesha kuchukizwa na maneno ya Rais wa shirikisho la soka la Ufaransa.MbappeKocha wa klabu ya PSG Christopher Galtier ameungana na Mbappe kwa kusema anaona staa huyo alikua sahihi kwani hata yeye anaamini Zidane ni mchezaji anaestahili heshima kubwa kwenye timu hiyo, Pia akiwa kama kocha amefanikiwa kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya mara tatu mfululizo. Galtier amesisitiza zaidi maneno yaliyozungumzwa yamezua hisia kali lakini inabidi watu wajue Zidane anahitaji heshima kubwa zaidi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa