Staa wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe anatajwa zaidi kama mrithi wa kitambaa cha unahodha alichokua akikivaa Hugi Lloris aliestaafu siku ya jana.

Hugo Lloris ambaye alikua nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa kwa muda mrefu jana alitangaza kustaafu timu hiyo. Vyanzo mbalimbali kutoka nchini Ufaransa vinaeleza kua nyota Kylian Mbappe ni mchezaji anaetazamiwa zaidi kua nahodha mpya wa timu hiyo.MbappeMchezaji huyo mwenye miaka 24 anapewa nafasi kubwa ya kuuchukua nafasi ya Hugo Lloris kama nahodha mpya wa kikosi cha Les Blues, Lakini imeonekana watu wengi kutia shaka juu ya Mbappe wengine kudai umri wake bado mdogo kuongoza timu hiyo.

Kocha wa klabu ya PSG Christopher Galtier anasema hana hofu na mchezaji huyo kua nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa kwasababu ya umri wake, Kwani anaamini kigezo cha mchezaji kua nahodha kwenye timu ya taifa ni michezo ambayo amecheza kwa timu hiyo na Mbappe tayari amecheza michezo 66 na kufunga mabao 36 kwenye timu hiyo.MbappeTaarifa kutoka vyanzo mbalimbali nchini Ufaransa vinasema kua nahodha wa Manchester United Raphael Varane ni miongoni mwa wachezaji watakaotoa upinzani mkali kwa Kylian Mbappe kwenye kinyang’anyiro hicho, Kwani beki huyo amecheza michezo mingi kwenye timu hiyo huku akiwa nahodha msaidizi kwenye timu hiyo kutokana na ukongwe wake kwenye timu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa