Klabu ya Ajax Amsterdam imeendelea kua na msimu mbaya baada ya leo tena kupokea kichapo cha mabao manne kwa matatu dhidi ya klabu ya Utrecht katika ligi kuu ya Uholanzi.

Ajax wakiwa ugenini leo wameendeleza fomu yao mbovu ambayo wamekua nayo msimu huu kwenye ligi kuu nchini Uholanzi baada ya kupokea kichapo chao cha nne katika ligi hiyo msimu huu.ajaxMabingwa hao wa muda wote wa ligi kuu yas Uholanzi maarufu kama Eredivise wamekua na wakati mgumu sana tangu msimu uliomalizika, Wakiwa hawapati matokeo mazuri na kupelekea kupoteza taji la ligi hiyo msimu jana.

Msimu huu mabingwa hao wa zamani wa Uholanzi wameendelea pale walipoishia msimu uliomalizika, Huku ikionekana msimu huu hali ni mbaya zaidi kwani mpaka sasa wameshapoteza michezo minne kati ya saba waliyocheza msimu huu kwenye ligi hiyo.ajaxAjax wanakamata nafasi 17 wakiwa nafasi moja juu ya timu inayoshika mkia wakiwa na alama zao tano baada ya kushinda mchezo mmoja tu kati ya saba, wakipokea vichapo mara nne na kutoa sare katika michezo miwili ikiwa mchezo wao mwisho kushinda ulikua mwezi wa nane.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa