Hatua ya robo fainali ya Fifa Club World Cup imemalizika kwa Al Ahly kuwalaza Al-Duhail na sasa watachuana na Bayern Munich.
Miamba ya soka la Misri na Afrika kwa ujumla – Al Ahly walikuwa wakipambana na miamba ya soka la Qatari, Al -Duhail katika mchezo wa robo fainali.
Pengine mashabiki wengi walimshangaa kocha Mosimane kwa kumuanzisha mshambuliaji raia wa Congo, Walter Bwalya na kumuacha Marwan Mohsen benchi.

Bwalya alitoa pasi muhimu ya ushindi ambapo Hussein El Shahat aliitumia vizuri na kupachika goli la ushindi katika kipindi cha kwanza.
Kwa matokeo haya, miamba hii ya soka la Misri watavaana na mabingwa watetezi wa Bundesliga na Ligi ya Mabingwa, Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali.
Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.



Sania
Mpambano mkali sana
Magdalena
Itakuwa balaa sana
Sarah
Litakuwa bonge la mpambano
Adelta
Itapendeza Sana
Khadija
Itapendeza sana
Neema juma
Itakuwa bomba sana
Dorophina
Al ahly watawaweza kweli munich
Caroline
Al ahly wapo juu
Hopemwaikuka
Aisee pongez kwao
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri sana
Issa
Bonge la mech
warda
Hatari hii