Bosi wa Juventus, Andrea Pirlo amesisitiza kuwa yeye hana mpango wa kuachia ngazi klabuni hapo.
Juventus tayari wamepoteza taji la Serie A kwa Inter Milan, na baada ya kukubali kichapo cha bao 3-0 nyumbani dhidi ya AC Milan amesalia katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi.

Hatma ya Andrea Pirlo klabuni hapo imekuwa na sintofahamu, kukiwa na shinikizo kubwa la mahitaji ya mabadiliko klabuni hapo. Mameneja kadhaa, akiwemo Zinedine Zidane tayari wametajwa kutazamwa kama mbadala wa meneja huyo.

Hata hivyo, meneja huyu mwenye miaka 41 ambaye ameshinda mechi 30 na kutoa sare mecgi 10 na kupoteza mechi 8 kwenye jumla ya mechi 48 za ligi, anasema kuwa hana mipango ya kuachia ngazi.

“Sifikirii kustaafu, sina mipango ya kustaafu. Kazi yangu inaendelea licha ya ugumu uliopo, nitaendelea ikiwa nitaendelea kupewa nafasi na klabu.” –

Andrea Pirlo

Juve walianza kupoteza matumaini hasa baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Porto, na wanatarajia kuwa watarejea kwenye njia yao ya ushindi pale wanapowatembelea Sassuolo Jumatano.


Pesa Ipo Hapa Katika Kasino ya Lucky Lucky.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Andrea Pirlo, Andrea Pirlo Amesisitiza Hataachia Ngazi Juventus!, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa