Ukisikia siku ya kufa nyani miti yote huteleza, ndio maisha ya Antonio Conte na Inter Milan kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Inter kutopata ushindi kwenye mchezo wowote kwa mechi nne mfululizo kwenye mashindano ya Ulaya.

Antonio Conte ameshuhudia timu yake ikiambulia kipigo kingine kutoka kwa Real Madrid jana usiku. Matokeo ambayo yanaifanya Inter ishike mkia kwenye Kundi B wakiwa pointi 5 nyuma ya Madrid (nafasi ya 2) na pointi 6 nyuma ya vinara wa kundi hilo  Borussia Monchengladbach.

Baada ya kipigo hicho (2-0), kocha Antonio Conte atoaneno. Conte ameiambia Sky Sport Italia “siku zote itaendelea kuwa ngumu kucheza na timu kama Real Madrid kwa hiyo unapokuwa umeshafungwa goli moja na unapungufu ya mchezaji mmoja, unakuwa na kazi kubwa ya kuupanda huo mlima.

“Ninadhani tumeona tofauti yao na sisi. Isituvunje moyo, imetuonesha ni njia gani tunapaswa kuifuata.

“Tunatakiwa kuwawatulivu na kuongeza juhudi zaidi, tutambue ni wapi tupo  na tusiyumbishwe na maneno ya watu wa nje.

“Njia sahihi zaidi ni kufanya kazi kwa bidii na kukua kwa kila linalowezekana.”

Kupoteza mchezo dhidi ya Madrid kunayaweka matatani matarajio ya Inter kufuzu hatua ya 16 bora. Mpaka sasa Inter wanapointi 2 pekee katika michezo 4 waliyocheza.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa