Zinedine Zidane amekuwa akifurahishwa sana na kazi ya Lucas Vazquez, huku akiamini kuwa ‘Real Madrid ipo moyoni’ mwa nyota huyu. Anafikiri zawadi tosha ni kumpa mkataba mpya aendelee kutoa huduma klabuni hapo.

Nyota huyu ameanza katika gemu saba za Real Madrid msimu huu wakati mkataba wake ukiwa unaelekea ukingoni mwishoni mwa kampeni.

Kwenye gemu ya Jumatano dhidi ya Inter Milan Vazquez alikamilisha dakika 90 dimbani wakiondoka na ushindi wa 2-0 wa Ligi ya Mabingwa. Alibamba zaidi kwa kwa ushambuliaji wake wa moja kwa moja.

Vazquez pia alikuwa na mashuti mengi kuliko mchezaji yeyote uwanjani akifikisha mashuti 4 kwa gemu nzima. Kimsingi amekuwa sehemu muhimu ya ushindi wa Real Madrid.

Lucaz Vazquez

Vazquez ameonyesha uhodari wake kwa kutokea upande wa beki wa kulia wakati mwingine na Zidane anataka staa huyu miaka 29 atakuwa msaada kwa Real, ni vyema azawadiwe mkataba mpya.

“Sasa anayo nafasi ya kutuonyesha kile alichokuwa nacho. Alikuwa mchezaji wa timu ya vijana hapa kwetu na Madrid ipo moyoni mwake. Nina furaha kwake na timu.”

Zidane anamuona kama ni mchezaji anayejitoa sana na yeye kama kocha anathamini mno mchango wake uwanjani na nje ya uwanja kama miongoni mwa wachezaji bora kikosini. Bila shaka Real watampa mkataba mpya hivi karibuni.


 

USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

18 MAONI

  1. Lucas Vazquez umri umemutupa mkono, ana muda mfupi kuendelea kusakata kabumbu. Baada ya kuondoka wachezaji wakongwe na mahiri nae amepata nafasi ya kucheza

  2. Vazquez ameonyesha uhodari wake kwa kutokea upande wa beki wa kulia wakati mwingine na Zidane anataka staa huyu miaka 29 atakuwa msaada kwa Real, ni vyema azawadiwe mkataba mpya.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa