Hansi Flick amemuelezea mlinda mlango wa Bayern Munich Manuel Neuer kama “Mtaalamu” baada ya kuonesha kiwango kikubwa siku ya Jumatano katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Salzburg kwenye michuano ya Champions League.

Robert Lewandowski, Kingsley Coman na Leroy Sane walitupia wavuni kwa upande wa timu ya Bayern Munich ambayo mchezaji wake Marc Roca alitolewa nje kwa kadi baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano kipindi cha pili cha mchezo.

Hansi Flick Apagawa na Kiwango cha Golikipa Neuer.
Wachezaji wa Bayern Munich wakisherehekea goli.

Matokeo hayo yameisadia Bayern Munich kukamilisha ushindi wa nne katika michezo minne kwenye kundi A na kukamilisha hatua ya makundi.

Huenda matokeo yangekuwa mabaya kwa upande wa Bayern kama zisingekuwa juhudi za Neuer, ambaye aliokoa mashuti kumi kutoka kwa timu ya Salzburg ya nchini Austria baada ya kuokoa michomo ya Berisha na Enock Mwepu.

“Manu amekuwa na kiwango kizuri miaka mingi,” aliiambia Sky Sport. “Akiwepo uwanjani nafasi ya washambuliaji kupata magoli inakuwa ni ndogo sana.

“Yupo katika kiwango kikubwa katika maisha yake ya soka ni mtaalamu sana na ana malengo na kazi yake”.

Flick hakufurahishwa sana na kiwango cha wachezaji wake baada ya kuonekana wakipoteza sana mipira lakini amesisitiza watafanyia kazi mapungufu aliyo yaona.

“Tulitengeneza ugumu kwa sababu tulipoteza mipira sana, mpira kupotea haitakiwi hili litokee kama hivi tena tunakuwa tupo kwenye hatari ya kuruhusu kushambuliwa.

Neuer pia alikubaliana na Flick kwamba possession ya Bayern ilikuwa nyepesi lakini anaamini ni muhimu walipata ushindi na kukumbuka kwamba wamefikia lengo la kusonga hatua inayofuata.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

18 MAONI

  1. Bayern Munch wana golikipa bora sana tukumbuke msimu ulio pita aliyo yafanya kwenye timu yake alikuwa goli kipa bora sana

  2. Neuer pia alikubaliana na Flick kwamba possession ya Bayern ilikuwa nyepesi lakini anaamini ni muhimu walipata ushindi na kukumbuka kwamba wamefikia lengo la kusonga hatua inayofuata.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa