Real Madrid wameripotiwa kuwa wanamuaona mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku kama mbadala wa muda mrefu wa Karim Benzema.

Lukaku amekuwa katika fomu nzuri kwa klabu yake ya Italia tangu kuanza kwa kampeni ya msimu huu 2020-21, akipata magoli mara tisa katika mechi tisa za mashindano yote.

Wakati huo huo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amefunga jumla ya mabao 43 katika mechi 60 tu akiwa na kikosi cha Antonio Conte tangu alipowasili kutoka Manchester United msimu wa joto wa 2019.

Romelu Lukaku Kuwa Mbadala wa Benzema Real

Benzema bado ni mchezaji muhimu kwa kikosi cha Zinedine Zidane, lakini Mfaransa huyo atakuwa na umri wa miaka 33 mwezi ujao, na Los Blancos wanafikiria kuangalia mbadala wa mshambuliaji huyu wa muda mrefu.

Kulingana na ripoti huko Uhispania, rais wa Madrid Florentino Perez anamwona Lukaku, ambaye ana kandarasi San Siro hadi mwisho wa kampeni ya msimu wa 2023-24, kama mbadala anayeweza kusainiwa.

Mchezaji huyo wa miaka 27 anadaiwa alikuwa kwenye rada za uhamisho za Manchester City msimu wa joto. Huenda safari yake ikaendelea upande wa La Liga.


 

USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa