Zinedine Zidane amesema kwamba Lucas Vasquez “Ana Real Madrid ndani ya moyo wake” na anastahili kupewa ofa ya mkataba mpya na klabu.

Mchezaji huyo wa Spain ameanza katika michezo saba ndani ya Madrid msimu huu lakini anaelekea ukingoni mwa mkataba wake na Real Madrid.

Zidane: Vazquez Anastahili Mkataba Mpya Real Madrid.
Mchezaji wa Real Madrid, Lucas Vasquez.

Alicheza dakika zote tisini siku ya Jumatano mchezo wa Madrid dhidi ya Inter na Madrid kuibuka na ushindi wa 2-0 kwenye michuano ya Champions League.

Alimtengenezea asisti Rodrygo aliyetokea sub na kufunga goli la pili baada ya Eden Hazard kufunga goli la mapema kwa mkwaju wa penati, Vasquez alipiga mashuti manne idadi kubwa kuliko mchezaji yeyote aliyekuwepo uwanjani.

“Mara nyingi amekuwa akitupa kila kitu, nimekuwa nikithamini kile anachotupa dimbani,” Zidane aliiambia Movistar+.

“Sasa ana fursa ya kutuonesha kile alichonacho alikuwa mchezaji mdogo na madridi ipo ndani ya moyo wake, nina furaha naye na timu pia.

“Nimchezaji muhimu sana na klabu inalitambua hilo,nadhani atapewa mkataba mpya.”

Penati aliyopiga Hazard dakika ya saba ya mchezo ilimfanya mfunge goli lake la kwanza katika Champions League tangu mwaka 2017 katika mchezo wake wa nne ambao ameanza.

“Tumecheza mpira mkubwa kuanzia kipindi cha kwanza mpaka mwisho,” Zidane alisema “Nina furaha na wachezaji pale wanapo amua kukiwasha wana kiwasha.”


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

20 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa