Kocha wa klabu ya Tottenham Antonio Conte anaamini kuwa inahitajika kazi ya ziada kufanyika ikiwa timu yake itataka kushika nafasi ya nne japokuwa yuko nyuma ya alama tatu zidi ya Arsena ambaye anashika nafasi hiyo.
Kikosi cha Antonio Conte kwa sasa kinashika nafasi ya tano nyuma ya Arsenal, ambaye siku ya jumatatu anaenda cheza na Crystal Palace, huku Spurs akicheza na Newcastle wikiendi hii.
Conte bado anaimani ya kuwa anaweza kumaliza kwenye nafasi nne za juu na alipoulizwa kuhusu tumaini la Spurs kumaliza nafasi nne za juu alijibu, “ni sawa kuandika malengi yako, ni ngumu ngumu sana. Sisi sio timu pekee ambayo tunata hiyo nafasi, kuna arsenal ambaye kwa sasa ana nafasi na pia kuna United.
“United ni timu kubwa ambayo msimu huu imekuwa ikipambana sana, msimu ulioisha ilikuwa Liverpool. Vinginevyo uingereza, narudia tena, unacheza kwa malengo ya wengine. Kwa sababu kuna timu nne, yoyte ambaye yuko juu kwa wakati huo ni klabu yenye nguvu kuliko nyingine, kwa sababu nyingi.
“Kwa msimu huu inategemewa Man Utd, ila sisi ni moja ya timu ambazo tunajaribu kuichukua hiyo nafasi. Ikiwa utaniuliza mimi kuhusu huko myuma kuweza kuipata hiyo nafasi ya kuweza kucheza ligi ya mabingwa ulaya, ningekwambia ni ngumu ngumu sana.”
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.