Klabu ya Arsenal ipo kwenye mazungumzo na kocha wake Mikel Arteta kwajili ya kumuongezea mkataba kutokana na kazi nzuri ambayo amekua akiifanya klabuni hapo.
Kocha Mikel Arteta amekua na wakati mzuri ndani ya klabu ya Arsenal jambo ambalo limewavutia mabosi wa klabu hiyo kuhitaji kuendelea kubaki na kocha huyo ndani ya klabu hiyo kwa miaka mingi zaidi.Kocha Mikel Arteta amekua na misimu miwili bora sana ndani ya klabu hiyo tangu akabidhiwe timu hiyo mwaka 2019 mwezi Disemba, Kutokana na ubora ambao ameuonesha kocha huyo kumemfanya kua moja ya makocha wenye thamani kubwa kwasasa sokoni.
Taarifa zinaeleza kama watafikia makubaliano baina ya pande zote mbili ya kuongeza mkataba kocha Mikel Areta anaweza kua moja ya makocha ambao wanalipwa zaidi kwasasa barani ulaya kutokana na kiasi ambacho atakipokea baada ya kusaini mkataba mpya.Klabu ya Arsenal imekua kwenye kiwango bora sana na kuelezwa moja ya timu bora kwasasa barani ulaya, Huku ikiwa ni kazi kubwa ambayo imefanywa na kocha Mikel Arteta na ndio sababu kubwa ya mabosi kutaka kumbakiza kocha huyo ndani ya viunga vya Emirates.