Arsenal wamekamilisha usajiri wao wa kwanza tokea dirisha la usajiri lifunguliwa kwa kumchukua kinda kutoka nchini Brazili aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Sao Paulo Marquinhos

Marquinhos mwenye umri wa miaka 19, ameigharimu klabu ya Arsenal kiasi cha £3million kama ada ya uhamisho, huku akitarajiwa kuwa mbadala wa muda mrefu kwenye klabu hiyo na atajiunga na klabu kwenye safari ya “pre-season” nchini Marekani .

Arsenal

Awali kuulikuwa na tetesi kuwa kinda huyo alikuwa karibu kujiunga na klabu ya Wolves na tayari walishakubaliana na mchezaji huyo kabla ya mkurugenzi wa ufundi Edu kufanikisha uhamisho huo.

“Tunafuraha kukamilisha uhamisho wa Marquinhos kutoka Sao Paulo, mchezaji ambaye tulikuwa tunamfuatilia kwa muda mrefu. Edu alinukuliwa akisema baada ya kufanikisha deal hilo.

“Miaka 19 ni bado mdogo sana, ni mchezaji wa baadae. Tunatarajia Marquinhos atajiunga nasi kwenye pre-season, kwenye makazi yake mapya, na ataendelea kukua na kuboresha kiwango chake nasi”


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa