Mauricio Pochettino zama zake ndani ya klabu ya PSG zimekweishwa na ameshaoneshewa mrango wa kuondoka nchini Ufaransa na jiji la Paris ni muda wa kupanga mabegi na kutafuta kituo kinachofuata, je Hispania ni kituo sahihi kwake?

Huenda inaweza isimchukue muda mrefu kupata kazi kutokana na CV yake, lakini kuna Offer Mauricio Pochettino ameahidiwa na mgombea uraisi wa klabu ya Athletic Bilbao Ricardo Barkala ikiwa atashinda kiti hicho, basi simu ya kwanza kabla hajakabidhiwa Ofisi na kwa Pochi.

Mauricio Pochettino

Klabu ya Athletic Bilbao inatarajia kufanya uchaguzi wa raisi June 24 na Ricardo Barkala ni miongoni mwa wagombea wanne wa nafasi hiyo. Iwapo atafanikiwa kuwa raisi wa klabu hiyo atahakikisha anamchagua Ramon Plane kuwa mkurugenzi wa michezo ili iwe kazi nyepesi kwa Pochettino kwani awali alishafanya kazi nae akiwa Spurs na Espanyol.

Athletic Bilbao kwa sasa haina kocha na inahitaji kocha mpya baada Marcelino kuachana na klabu hiyo baada ya msimu kuisha, na jina linalotajwa sana ni Mauricio Pochettino ndio anayeoneka kuwa anaweza kuirudisha klabu hiyo kwenye ramani ya soka la nchini Hispania.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa