Arsenal Wamchukua Raya Rasmi

Klabu ya Arsenal sasa ni rasmi wamefanikiwa kumchukua aliyekua golikipa wa klabu ya Brentford David Raya ambaye wamekubaliana kiasi kinachokaribia paundi milioni 30na klabu hiyo.

Davida Raya atajiunga na Arsenal baada ya makubaliano ya pande zote mbili ya mchezaji na klabu yake vilevile, Hivo washika mitutu hao kutoka jiji la London wanakwenda kumiliki magolikipa wawili wenye ubora mkubwa.arsenalGolikipa David Raya ambaye toka mwanzo alihitaji kujiunga na vijana wa Mikel Arteta kuelekea msimu ujao, Kwani kipa huyo alishahitajika na vilabu vya Tottenham pamoja Bayern Munich lakini haikuwezekana.

Katika milingoti ya Arsenal msimu ujao kunatarajiwa kua na yshindani mkubwa, Kwani golikipa Aaron Ramsdale alikua na msimu bora sana ndani ya klabu hiyo huku Raya nae akiwa moja ya magolikipa bora kwenye ligi kuu ya Uingereza.arsenalWashika mitutu kutoka jiji la London wameonesha nia ya dhati ya kuendelea walipoishia msimu uliomalizika, Kwani klabu hiyo imeshafanya usajili wa wachezaji takribani wanne mpaka sasa na kutumia kiwango kikubwa cha pesa kuliko msimu wowote.

Acha ujumbe