
Kocha mkuu wa timu ya Arsenal Mikel Arteta amesema angependa kumbakisha David Luiz katika kikosi cha timu hiyo licha ya kuwa kandarasi itafika tamati mwishoni mwa msimu.
Arteta anamtaka beki huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea David Luiz kusalia Emirates, amekuwa akiwasukuma wachezaji wenzake imekua ikisaidia kuwaunganisha kucheza kitimu na kuzingatia mchezo.
David Luiz mwenye umri wa miaka 33 anacheza katika safu ya ulinzi amekua na umuhimu katika kikosi cha washika mitutu hao.

“Nina furaha sana kuwa na David Luiz katika timu, nataka abaki nasi amekuwa akinihamasisha ni mtu muhimu katika timu yetu” alisema Arteta.
Mbrazaili huyo alihamia katika timu ya Arsenal akitokea kunako klabu ya Chelsea mwaka uliyopita, tayari amesha ichezea Arsenal mechi 32 kwa msimu huu.
Arsenal watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Manchester City siku ya Jumatano ambapo City watawakaribisha Arsenal, katika dimba la Etihad kwa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.
Mpema siku hiyo hiyo ya jumatano Aston Villa wata wakaribisha Sheffield United katika uwanja wao wa nyumbani, Villa wana hitaji kupata matokeo ili kujinusuru katika mstari wa kushuka daraja
Arsenal wapo nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi ya EPL wakiwa tayari wamecheza mechi 28 na kujikusanyia alama 40. Walipoteza kwa goli 2-3 katika mchezo wao wa kirafiki waliyocheza dhidi ya Brentford.


Njiku
Arteta nikocha mzuri kwa arsenal pia nikocha mchezaji hivyo bhasi kwa uwezo aliekuwa nao David luiz kwenye safuu ya ulinzi ipo juu kwa arsenal na hakuna kama yeye pale arsenal pia anahamasisha timu akuna asiemjua David luiz maana kakipiga sana club ya chelsea
Issa
Luiz ni beki bora sana abaki hapo
Caroline
David Luiz akibaki arsenal itapendeza zaidi
lombo
maneno matupu hayasaidii kama unamtaka mwongezee mkataba na si maneno
Neema
Luiz abakie tu the gunners zaidie kikosi
Devotha
Luiz ni mchezaji mahiri sana
Salma
Ilo ni jembe wamuongeze mkataba abaki tyu
Sadick
Luiz umri umeenda na hajatengeneza chemistry nzuri, back-line mbovu inavuja. Wacha aondoka tu na Arteta atafute mbadala#meridianbettz
Magdalena
Abaki atulie acheze mpira
Johnmary joel
Hakika ni mchezaji mzuri mpeni mkataba wa kudumu#meridianbettz
felister
yeye mwnyw ana maamuzi yake binafsi akitaka kuondoka arteta huwezi mzuia kwa chochote
Genia Sikaluzwe
Luiz ni mchezaji mzuri wa mpira
Leonard
Ni mchezaji mzuri
Dorophina
Luiz yupo vizuri Ni bora angebaki arsenal bado wenzie wanamuhitaji
Mwanaidi
Huyo mshikaji umri umeshaenda
Theckla
Yuko vizuri
Evaluziga
Abaki asernal itakuwa vizuri
Genia Sikaluzwe
Abaki tu asernal itakuwa poa sana
Ernest
Luiz kashajichokea atatoa maboko huyu
Antony Luseno
Arteta yupo sahihi unabidi luiz abaki adhiririshe ubora wake kama alivyokuwa Chelsea zama hizo
David Pere
Bado anafaa kwa kiwango chake maana hawana pesa za kumnunua beki mwingine
Fatuma kasomo
Yuko vizur abaki tu
Elika
Hapo ndipo panapomfaa hivyo basi.aendelee kubakia hapo hapo asiyumbe
Mwanahamisi
Yuko vizuri
Khadija
Luiz ni mchezaji mzl sana#meridianbettz
Gabriel
Kwa upande wa arteta yuko sahihi kwa alichokiongea maana bek huyu yuko vzur ila nae anauhuru wa kuchagua
isha
Abaki tuu
Haulath/Lath graaffix
Yote kheri
Haulath/Lath graffix
Yote kheri
Hamidu
Beki kisiki! Bado ni mchezaji muhimu#meridianbettz
christopher
Mimi naona aende tu huko ureno, kwa namna moja au nyingine amekuwa ndio sababu ya magoli mengi wanyofungwa arsenal
JULIANA
David Luiz abaki tu
Ester jackson
Kwa umri alio nao luiz unakimbilia kustaafa bila chochote cha kukumbuka kama anataka kufanikiwa aondoke arsenal na wala asiende Chelsea aende timu nyingine kubwa akapate mbinu zaidi ya mafanikio
Hope mwaikuka
Abak tu
Povel
Luiz abaki kwa kpnd hk kigumu thnks meridian bet kwa update
Shafii
Arteta yuko sahihi kwa umr aliokua nao Ruiz ni Bora akamalizie career yake the gurnars
Mwajuma
Bora abaki tu kwasababu arsenal bado wanamuitaji
Tahiya
Arteta yuko sahihi kwa sasa Luiz bdo anahitajika kwa Arsenal
Zeiyana
Nadhani ateta kaona kuna umuhimu wa kufanya kazi na Ruiz
Furahav
Beki mzuri.
Neema hassan
Luiz mchezaji mahiri
Emmy cleopa
Nichezaji mnzur sana
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo vizuri anajua
Aziza mushi
Yupo vizuri.